Mark 3:13-18

13 aIsa akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia. 14 bAkawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri 15 cna kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu. 16 dHawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro); 17 eYakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo); 18Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
Copyright information for SwhKC